USIOE AU KUOLEWA MAPEMA


*Usioe na kuolewa mapema:*

👉Mwanamke anayeolewa na kuzaa mapema anahatarisha afya yake kwa kuwa viungo vyake vinakuwa havijakamilika kuweza kuhimili mikiki mikiki ya kujifungua. Wengi ama hufa ama kupata maradhi au kusababisha matatizo kwa watoto wanaozaliwa wakati wa kujifungua. Wazazi wenye tabia ya kuwaoza watoto wao wangali wadogo waache mila na utaratibu huo maana unawanyima watoto wao haki ya kufurahia ndoa. Ukomavu wa viungo huenda sambamba na usalama wa viungo vyenyewe – na hasa viungo vya uzazi. Viungo vya uzazi vikitunzwa vyema huwa salama wakati wa uchumba lakini visipotunzwa huathirika kwa njia ya maambukizo na hatima yake ni kupata ulemavu wa kudumu au maradhi yasioyoponyeka. Maradhi kama ya saratani ya shingo imegundulika kuwa huweza kusababishwa na kujamiiana katika umri wa utotoni. Kanuni ya msingi kwa wavulana na wasichana ni kutoyachokoza mapenzi mpaka wakati muafaka utakapofika. “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe” (Wimbo Ulio Bora 2:7)


Post a Comment

0 Comments