UMUHIMU WA KUOMBEA TUMBO LA UZAZI
NA
UKOMBOZI WA TUMBO LA MWANAMKE
Tumbo la Mwanamke ni Madhabahu
Nguvu za Mungu zinazidi mawazo na fikra za mwanadamu
Tukiwa katika mwili ni vigumu kuwaaminisha watu mambo ya rohoni
Mwili ni adui wa nguvu sana ndo maana watu wengi wanashindwa kuyashinda mambo ya mwili.
Hatuwezi kufanya jambo pasipo nguvu za Mungu ndani yetu.
Yesu alijitambulisha kwa kumtambulisha Roho takatifu kwanza kwa kusema "Roho wa Mungu yu juu yangu"
Ukiwa mchanga katika roho kuna vitu Mungu hawezi kuvifanya ndani yako mapaka ukomae kiroho
Kuna hatua za kupitia ili ukomae kiroho.
Na hata ukifungua kanisa anayefanya kazi ni Roho mtakatifu na lazima akukomaze kiakili ili uanze kumuona akaifanya kazi ndani yako
Mahali penye Roho Mtakatifu Mungu anakupa mani ya kutulia.
Eneo ambalo mtumishi wa Mungu anaandaliwa siku zote ni akili maana hawezi kukaa kwenye akili changa.
Yesu Jambo la kwanza namtambulisha Roho mtakatifu maana najua pasipo Roho wa Mungu hataweza kufanya kitu chochote.
Matendo Ya Mitume 1:4
Na hata alipopaa aliwaambia wanafunzi wake wasiende mahali popote mapka wapokee Nguvu za Mungu ndani yao
Na walipopokea nguvu za Mungu waliweza kutoka na kuendelea kuifanya kazi ya Mungu na huu ujasiri uliwapa uwezo wa kuhubiri bila siri bali walihubiri wazi wazi
Jambo Kubwa tunalotakiwa kulitafakari kila siku ni Jinsi gani tunaweza kufanya na kuenenda katika nguvu za Mungu.
Roho Mtakatifu ni kama kitu kinachoweza kuditect kitu sehemu yeyote!
Tunatakiwa kuditect na kuzijua nguvu za Mungu ni kwa sababu hatuko makini na mambo tunayoyafanya.
Daudi akasema niondolee moyo wa jiwe! Unapokuwa na ditection ya aroho mtakatifu lazima masha yako yabadilishwe maana Roho Mtakatifu akiwepo ndani yake anamdhihirisha Yesu Kristo ndani yake.
Kila mtu amepitia kwenye eneo Linaloitwa tumbo la mwanamke kwa miezi tisa.
Tumbo la mwanmke ni madhabahu na madhabau ni eneo ambalo mtu anaweza kuwekwa
Roho za watu zinakaa madhabahauni
Madhabahu ziko mbili
1. Zinazoweza kumshikilia mtu kwa mema
2. Na madahabau za giza zinazotumwa ili kumfunga mtu
Kumtoa mtu madahabahuni inahitaji akili na nguvu zaidi
Kama Madhabahu ya Mungu ina Nguvu na hivyo hivyo ya iblisi shetani ina nguvu pia
kutokujua sheria haikusababishi usihukumiwe kwa kosa ulilofanya
Ezekieli 16;2
Wako watu wengi wanoteseka kwa sababu ya matumbo ya wanawake.
Mungu hakuweza kumleta Mkombozi wa ulimwengu kwa kumpitisha kwenye tumbo la mwanamke
Uwezi kuisaidia dunia bila kugusa eneo la tumbo la mwanamke, Tumbo lina uthamani wa kukomboa nchi nzima
Tumbo, nchi na ukombozi ni ndugu.
Mama yako akikulaani kwa kushika tumbo hauwezi kufanikiwa katika jambo lolote.
Matumbo ya wanawake yamebeba nguvu ya ukomboa kizazi kizima.
Wanawake wengine kuna vitu hawataki hasahasa suala la kumuheshimu mume wake, na uatakua na binti yake anakuwa hivyohivyo.
Kama tumbo la mwanamke limelaaniwa basi huwezi kufanikiwa chotote!
Kumbukumbu la Torati 28;4, 11
Una baraka za tumbo, Mungu anapotaka kumbariki mtu anagusa tumbo lake, unaweza ukabariki hata tumbo la mtoto mchanga na hata ambaye yuko kwenye mifupa.
Tumbo pia linaleta laana , tumbo limebeba hatma ya maisha yetu
Mwanamke akishakuwa mchawi anatumia tumbo lake kuzuia baraka zako kwa kutamka maneno tu!
Kwanini wamama wengi ndo wanongoza kwa magonjwa ya uzazi, shetani akishakamata tumbo ameshakuharibia mambo yako yote.
Lengo la shetani kukuwekea uvimbe ni ili utolewe kizazi
Kuna watu wanataabika kwasababu ya matatizo ya tumbo, kumbe ulipozaliwa laana iliachiwa juu yako.
Kila tumbo la mwanamke linaenda kukombolewa leo kwa Jina la Yesu. Tumbo lako likazae wafalme sasa kwa jjina la Yesu.
Ufunuo 12:1-13
Mungu alimuweka huyu mwanmke kanisani ili aweze kulilinda tumbo lake.
Yesu akakutoe katika kila laana ya tumbo la na ukakombolewe tumbo lako kwa Jina la Yesu.
Wiki Ijayo kuanzia Jumatatu tutaanza kuombea maombi ya tumbo la UZAZI, pia tutashughulikia Roho za Utasa kupitia Kristo Yesu. Nimesema nikupe hizi Dondoo walau nikipata neema nitakuja kuendelea na sehemu zijazo.
Usiache kumkaribisha na mwenzako katika blog yetu hii.
0 Comments