IWEKE HII AKILINI MWAKO KIJANA.

1: Daima tuko sawa na hatukubali kabisa kuonywa, kukemewa na kukaripiwa. Atuonyaye, kutukemea na kutukaripia anasomeka kama adui wa kumwepuka kwa gharama zote tena akizidi kutufuata fuata tunamwambia achana na maisha yangu, hayo ni yangu hayakuhusu wewe. 2: Tunapenda kuimba kanisani lakini hatusomi BIBLIA zetu nyumbani wala Kuomba. 3: Tumejaa tamaa, hamu ya kufanya ngono (Uasherati) na hisia ambazo sisi tunaziita upendo au mapenzi. 4: Tunataka tuwe na ndoa bora, lakini tunapokuwa tumefika umri wa miaka 25 tunakuwa tulishakuwa ndani ya mahusiano ya kimapenzi kwa miaka kumi tayari. Wakati mwingine tumeshakuwa na wapenzi wa kike na wa kiume hata kuliko wazazi wetu. 5: Ngono na matendo machafu ya kingono sasa ni sehemu ya mahusiano yetu na tunaiita Mahaba/Mapenzi. 6: Hatukosekani kwenye kumbi za starehe (Club, Disco,Vigodoro) na hatuonekani kwenye Ibada za mikesha mbalimbali 7: Hatulipi Zaka zetu wala kutoa Sadaka tukisingizia sisi ni wanafunzi. 8: Tunajiita wanawake wa Ki-Kristo lakini tunavaa kama waigizaji wa sinema, nusu uchi kama sio uchi kabisa halafu tunasema ndo mitindo ya mavazi ya kisasa bila kujali sisi ni BARUA YA KRISTO au USHUHUDA wetu na U-Kristo wetu unaathiriwaje. 9: Tunapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. 10: Kanisani utatuona tukiwa tumeinua mikono huku twaimba nyimbo za taratibu kama tunaabudu vile lakini kwenye simu zetu mifukoni mwetu kuna picha za wanawake waliyo nusu uchi na wengine uchi kabisa, nyimbo za muziki wa kizazi kipya, maisha ya kujirusha na kutumia na tuna namna nzuri ya kulielezea hilo na kulifaulisha. 11: Tunaishi maisha ya huku na huku na mtu asikuulize utasikia achana na kufuatilia maisha yangu. 12: Tukienda kanisani wala neno halituhukumu tena kwa habari ya maisha tunayoyaishi maana mioyo imefanywa migumu na udanganyifu wa dhambi na tuna kiburi kuliko Lewiathani. 13: Tunajidai tunamwabudu Bwana Madhabahuni Kwa Roho na Kweli Kumbe Huku Sirini Tunamkana kwa Matendo yetu machafu kwa kiasi cha kwamba hata yakiwekwa wazi machoni pa watu watashangaa na kuhuzunika. 14: Ni mahiri kwenda Location na kupiga picha lakini hatuna Uamsho ndani mioyo yetu wa kwenda Kuhubiri Injili ya Kristo na wengine waokolewe katika vifungo vya dhambi. 15: Tunao muda wa kutosha wa kuongea na wapenzi wetu mpaka usiku wa manane lakini hatuna Shauku na Kiu kama ya ayala ya kujawa Roho Wa Bwana na Nguvu Zake, na hatuna tena muda wa kuwa na Ibada Binafsi na kuimimina mioyo yetu kwa Bwana Yesu Kristo. 16.Kugombanisha wengine na kuweka chuki bila sababu ili kusiwe na ushirikiano. 17.Kutafuta maombi ya zima moto pale ulipoumizwa katika mahusiano na kupretend kumfuata Mungu kwa siku chache muda ukipita unarudi kwenye uchafu wa ngono. 18.Wakati wa shida utawatafuta watu wa kukuombea , ukipata mafanikio utagombana na wale waliokuvusha kwa kiburi cha fedha na jeuri ya pesa, miradi uliyoifungua ikipigwa akili inakurudi kuwatafuta wale waliokuvusha. 19.Ni rahisi sana kukosa kutuma sadaka katika ibada Lakini bando la mitandaoni hukosi, na tena unalitumia kufanya upuuzi na kutizama ngono, ukiambiwa jiunge telegram kupata mafundisho ya Mungu utasema huna salio Lakini katika status zako udaku umejaa wa kishetani. 20.Ujuaji mwingi na kutafuta ufahari wa kutafuta watumishi wenye najina na kupiga picha nao ili uonekane matawi ya juu kwa watu, huu ni ushamba!! Mtafute Yesu, majina ya watu au umaarufu wa watu sio kigezo cha kuingia mbinguni bali matendo yako. Kijana hizi ni Nyakati za Hatari Sana Badilika na Geuka Mlango wa Rehema Bado Uko Wazi.Mkaribie Yesu. Acha vya dunia !! 
SIKU NJEMA.......

Post a Comment

0 Comments