Utangulizi
Leo tunaendelea kujifunza juu ya tumbo la uzazi , na kumekuwa na vita kubwa sana katika uzao wa tumbo la Mwanamke hivyo ni vyema tukaanza kujifunza na kuchukua hatua. Tukumbuke pia wiki Ijayo tutakwenda kupiga Roho za Utasa na Mungu atafanya kwako usikate tamaa.
Somo hili ni la muhimu sana kwa wapendao kutimizwa kwa makusudi ya Mungu duniani
Zaburi:139.13
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi:139.14
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi:139.15
Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi:139.16
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Shalom .
Kwa bahati mbaya ni kwamba Shetani na ufalme wake wanajua sana habari za uzao wa wanadamu kuliko hata wenye kupewa huo uzao.
Mwanadamu hajijui yeye ni nani duniani , lakini Mungu anamjua na Shetani anamjua , wala mwanadamu mwenyewe hajielewi kabisa na ni wachache waliopata ufahamu wa kujielewa.
Kuna vita vya kiroho vinavyopambanwa usiku na mchana juu ya uzao wa matumbo ya wanadamu.
Shetani anafuatilia uzao wa mwanadamu kwa karibu sana kwa sababu ya rekodi zilizoko juu ya uzao wa matumbo ya wanadamu.
Rekodi nyingi zinaonyesha kuwa mara kwa mara Mungu anapotaka kupambana na malango ya ufalme wa Shetani huwa anaandaa viuno na matumbo ya wanadamu kwa ajili ya kuachilia uzoa ambao utatumika kama vyombo vyake vya ajabu sana vya kutimizia huo mpango wake mkuu duniani kote na kwa sababu hiyo tumbo la uzazi hugeuka na kuwa uwanja wa vita na utakuta kuna kuwa na mapambano mapema sana juu ya uzao ambao unatarajiwa kupitishwa kwenye tumbo la uzazi kama lango la kiroho la kuachilia vyombo vya ajabu vya kuushambulia ufalme wa Shetani.
Ni muhimu sana kuyaombea matumbo ya uzazi na sio lazima mpaka uingie ndani ya ndoa ndio uliombee hilo tumbo ,liombee kila wakati ,wakati umeolewa na wakati bado haujaolewa pia ,itakusaidia kufanyika vema sehemu ya kutimizwa kwa makusudi ya Mungu duniani.
Tumbo la Bikira Mariamu lilibarikiwa hata kabla ya kuolewa na Yusufu ; Mungu alisema nae juu ya tumbo lake hata kabla ya ndoa yake na Yusufu na kwa uweza wa Mungu lilibeba mwokozi wa ulimwengu mzima.
Zaburi ya 139:13-16; inatueleza mambo ya ajabu sana pale, inasema tangia kwenye matumbo ya mama zetu , Mungu huwa anaumba makusudi yake ndani ya uzao wa hayo matumbo.
Kwa hiyo kulingana na Biblia ni kwamba Mungu anapokuwa anaumba uzao tumboni ,huwa haumbi tu uzao peke yake ,huwa anaumba uzao jumlisha na makusudi ndani ya huo uzao oooh haleluya haleluya.
Kwa hiyo usipende tu kuomba Mungu akupe tu uzao ,mwambie nipe uzao + makusudi mazuri na mema toka kwako ndani ya huo uzao.
Ni mambo yenye vita kweli kweli na ukianza kuomba maombi ya namna hii ,utaanza kuona mambo ya rohoni ya ajabu sana juu ya uzao wa tumbo lako na utabakia kushangaa.
Roho Mtakatifu ananionyesha mama mmoja wakati huu, akiwa na mimba alafu akaota ndoto , ya kuona nyoka akija na kulizunguka au kulizengea tumbo lake lenye mimba , sikia Roho ya Mungu inakujulisha juu ya vita iliyoko katika ulimwengu wa kiroho toka kwa Shetani juu ya huo uzao wa tumbo lako, hakikisha unapata msaada wa kimaombi kwa hali yako ,ili Mungu aachilie ulinzi juu ya huo uzao wako na ujifungue salama , maana haujabeba tu uzao bali ni uzao + kusudi la Mungu ndani yako; hauendi kuzaa tu mtoto ,bali unaenda kuzaa kusudi la Mungu kubwa sana na la ajabu duniani.
Ukisoma 👇
Ayubu:3.10
Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu. Wala kunifichia taabu machoni.
Nataka uone kitu kupitia hiyo mistari hapo ,tazama neno hili 👇
"haukuifunga milango ya tumbo la mamangu."
Tumbo la mama lina milango ya kiroho.
Milango hiyo Shetani anaweza kuitumia vibaya kama tusipojua namna ya kuiombea kwa umakini sana.
Ayubu anatueleza kuwa milango ya tumbo la uzazi inaweza kufungwa kabisa.
Na kwenye sehemu ya 2; tutaona aina mbalimbali
za ufungwaji wa matumbo ya uzazi na utashangaa sana mambo yanayokuwa yakifanywa huko ndani.
Tutaona na shuhuda za watu ambao nimepata nafasi ya kuombea matumbo yao ya uzazi.
Somo hili ni la muhimu sana kwa wapendao kutimizwa kwa makusudi ya Mungu duniani
Zaburi:139.13
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi:139.14
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi:139.15
Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi:139.16
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Tuangalie aina za ufungwaji wa matumbo ya uzazi.
Ukisoma Ayubu 3:10a; utaona ikisema hivi ; "Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu."
Ikimaanisha kwamba milango ya matumbo ya uzazi inaweza ikafungwa kwa sababu mbalimbali.
Sasa iko hivi milango ya matumbo ya uzazi inaweza kufungwa na Mungu mwenyewe kwa sababu zake binafsi na pia inaweza ikafungwa na Shetani kwa sababu zake binafsi.
Mungu akiifunga milango ya uzazi ya mwanadamu huwa anakuwa na kusudi lake maalumu.
Pia na Shetani akiifunga milango ya uzazi ya mwanadamu huwa na kusudi lake binafsi na mara zote , la kwake huwa ni la kupambana na mapenzi au makusudi ya Mungu yaliyokusudiwa kupitia ule uzao wa tumbo.
Kwa hiyo aina zote za ufungwaji wa matumbo ya uzazi ; unategemeana na upande upi umeamua kuyafunga hayo matumbo na makusudi yao juu ya huo ufungwaji wa hayo matumbo.
Ukisoma Biblia utaona suala la kufungwa kwa matumbo ya uzazi linatajwa kwa wazi wazi sana kwa sehemu tofauti kuwa Mungu ndie aliyekuwa akifunga hayo matumbo.
Lakini ni ngumu sana kuona Shetani akitajwa kwa wazi wazi kuwa ndio muhusika mkuu wa kufungwa kwa matumbo ya uzazi.
Ilinifanya nitafakari sana kwa kina kwanini Biblia haimtaji Shetani kama muhusika wa kwanza moja kwa moja.
Mungu akanisaidia kufahamu jambo katika kusoma vema Biblia na likanipa jibu ambalo natamani nawe ulifahamu vizuri pia.
Twende kwenye kitabu cha Mwanzo ,ukisoma kwenye 👇
Mwanzo:1.27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo:1.28
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Utaona kuwa mtu ni roho , na hiyo roho ilipoumbwa iliumbwa moja kwa moja na baraka ya aina ya uzazi.
Baraka ni nguvu ya kiroho yenye kuleta mafanikio juu ya jambo fulani ,kwa mfano jambo la kupata uzao wa tumbo.
Kwa hiyo hakuna roho ambayo iliumbwa pasipo baraka ya kupata uzao , roho zote ziliumbwa hivyo na ndio maana hata kichaa wa barabarani anaweza kubeba mimba na akapata uzao kabisa ,kwa sababu ndani yake iko roho yenye baraka ya kupata uzao wa tumbo.
Sasa sikia hapa ndipo tunapopata sababu kwanini Biblia haimtaji Shetani kama muhusika mkuu wa kufungwa kwa matumbo ya uzazi ,na badala yake inamtaja zaidi Mungu kwa sehemu nyingi sana ,kwa sababu baraka ya uzazi ni neno lenye kuamuriwa kwa nguvu na uweza wake binafsi ambao hakuna anayeweza kuupinga kabisa na kama Shetani angekuwa na uwezo wa kuupinga angekwisha zuia watu dunia nzima wasizae watoto kabisa na anajitahidi kupamba hapa kila siku ,usiku na mchana lakini hii nguvu ni nzito kwake sana.
Sasa sikia kinamfungulia Shetani njia ya kupenya ndani ya malango ya uzazi wa watu ni mazingira ya laana ambayo kwa namna moja au nyingine ,huyo mtu anakuwa ameyatengeneza kwa kujua au kwa kutokujua kabisa; lakini kiukweli hakuna mtu chini ya jua ambaye hana uzazi ndani yake kabisa.
Ndio maana usipate shida na kujisikia kukata tamaa kama ndani yako bado lango lako la uzao halijafunguka na hauna uzao ,Mimi nakueleza kuwa suala la kupata uzao ni haki yako kabisa , rudi mbele za Mungu kwa maombi ,inawezekana kabisa kukawepo na mazingira ambayo yameleta kufungika kwa lango lako la uzao. Mfano Vifungo vya ukoo ,Uchawi, Utoaji Mimba ,kutokumtii Mungu n.k
Shetani anatumia mazingira kubana uachiliwaji wa uzao
wa matumbo ndani ya watu.
Laana ni nguvu ya kiroho inayokuja kwa mtu kwa lengo la kuachilia hali za kutokufanikiwa na maharibifu katika maisha yake katika maeneo tofauti tofauti ,kwa mfano eneo la uzazi.
Shetani anatumia mazingira ya laana na n.k kupambana na mtu juu ya kupata uzao.
Haiwezekani mtu akose uzao wa tumbo kama ana mahusiano mazuri na Mungu hata kama ndie yeye amefunga hilo tumbo ,lazima atakuja kulifungua tu kwa wakati husika na usiache kuliombea tumbo lako.
Ukisoma 👇
Hesabu:5.27
Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosa mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake.
Hesabu:5.28
Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana.
Hesabu:5.29
Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;
Hesabu:5.30
au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za Bwana, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote.
Utaona habari ya mwanamke ambae mumewe aliingiwa na roho ya wivu kwamba anamuhisi mkewe amefanya uzinzi nje ya ndoa na yule mume akaenda kumshitaki kwa kuhani mkuu na kuhani mkuu alipewa maelekezo na Mungu juu ya kuhukumu mwanamke ambaye ametoka nje ya ndoa yake , na waliweka kipimo cha kujaribu kujua kama kweli mwanamke alitoka nje ya ndoa yake au ni roho ya wivu tu ndani ya mume.
Na katika kumjaribu ili wapate nafasi ya kumuhukumu utaona walikuwa kwanza wanatengeneza aina fulani ya laana kupitia maji ya uchungu ambayo mwanamke alikuwa akinyweshwa.
Laana ilikuwa ikimwingia mwanamke kama kweli alitoka na kwenda kufanya uzinifu nje ya ndoa yake na ile laana ilikuwa ikikimbilia moja kwa moja ndani ya tumbo la mwanamke la uzazi na ilikuwa inakwenda kutengeneza uvimbe ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke ikiwa kweli kama alitoka nje ya ndoa na kufanya uzinifu.
Kitu ninachotaka ukione hapo ni kwamba Mungu hapo wala sio muhusika wa kufungwa kwa tumbo la mwanamke moja kwa moja bali ni nafsi ya mume na mke ndio wahusika wakuu na mazingira yaletayo laana kwenye tumbo la uzazi wao.
Mungu hapo wala hana shida na hilo tumbo yeye ameweka sheria kwamba ikiwa watu binafsi watajijengea maziñgira ya kujiletea laana basi na Yeye atakaa pembeni na kupisha nguvu ovu au mbaya kutenda kazi ndani ya hilo tumbo la uzazi.
Utaona kwanza roho ya wivu ikitokea ndani ya mume na ile roho ya wivu inakwenda na kuinua mashitaka mbele za Mungu dhidi ya mkewe , na yale mashitaka yanatazamwa mbele za Mungu kama ni ya kweli au la na kama ni ya kweli tumbo la uzazi la mke lilifungwa na hakupewa nafasi ya kuwa na uzao tena kati ya ndugu zake.
Sasa unaweza kuanza kuelewa kwa nini ndoa yako haina uzao.
Sababu haiko kwa Mungu kabisa ,sababu iko kati yenu wawili , pengine mmoja wenu au wote mnahusika na kutengenezwa kwa mazingira ya kutokupata uzao wa tumbo.
Kwenye ile hesabu 5:27-30; utaona mume alikuwa na roho ya wivu na mke alikuwa anashikiliwa na jambo la uzinzi.
Vyote vinatumika kupambana na lango lao la uzao.
Endelea kuombea somo hili ,
Somo hili ni la muhimu sana kwa wapendao kutimizwa kwa makusudi ya Mungu duniani.
Zaburi:139.13
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi:139.14
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi:139.15
Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi:139.16
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Tulisoma Ayubu 3:10a; tukaona ikisema 👇
"Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu."
Ikimaanisha kwamba milango ya matumbo ya uzazi inaweza ikafungwa kwa sababu mbalimbali.
Na nilikuchambulia kwamba ufungwaji wa matumbo ya uzazi uko wa pande mbili ,yaani upande wa Mungu mwenyewe na wa upande wa Shetani.
Pande zote hizo hufunga matumbo wakiwa na sababu zao husika.
Na nikaeleza kwamba Shetani huwa anatumia mazingira kama ya laana na n.k kuyafunga matumbo ya uzazi na kiukweli ni kwamba Shetani sio mhusika mkuu wa ufungwaji wa matumbo ya uzazi ,mwenye mamlaka ya hayo matumbo ni Mungu binafsi ,kwa sababu alipoumba mtu ,alimuumba ndani yake na nguvu za kupata uzazi yaani baraka ya kupata uzazi ,tayari na kwa sababu hiyo mtu ni roho ambayo ndani yake kuna baraka ya uzazi tayari na haina haja ya kuangaika na jambo la uzazi ,kwa sababu tayari ilishaumbwa nalo ndani kwa ndani.
Kwa hiyo Shetani anadandia tu kazi ambayo sio ya kwake ,anachokifanya yeye ni kutazama kama kuna mazingira ambayo huyo ameyaruhusu ya kusababisha kuwepo kwa laana juu ya uzazi wa tumbo lake.
Embu tusome hapa tuone jambo 👇
Kumbukumbu La Torati:7.14
Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.
Utaona mazingira ya baraka huwa yanafukuza hali ya utasa.
Mazingira ya laana huleta hali ya utasa ndani ya matumbo ya uzazi.
Tazama maneno haya , uone kitu hapo 👇
Ayubu:15.34
Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
Ayubu:15.35
Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeneza udanganyifu.
Inasema jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa.
Neno jamii ni ukoo au familia.
Kutokumcha Mungu ni aina mojawapo ya mazingira yenye kusababisha utasa au kufungwa kwa uzao kwa watu.
Sasa katika mazingira ya namna hiyo sasa ndipo Shetani anapokuwa akipata nafasi kubwa ya kuyafunga matumbo ya uzazi na hata kuharibu mimba nyingi.
Ni vigumu sana kuwa mcha Mungu alafu uishie maisha yako katika kukosa uzao wa tumbo.
Kwenye kumcha Mungu ,Mungu mwenyewe atahakikisha uzao unatokea hata kama umri wako umekuwa kama wa Sara, lazima Isaka wako atokee tu oooh haleluya haleluya, atasakwa na kuchimbuliwa kokote alikofichwa mpaka atokelezee kabisa, kwenye kumcha Mungu kuna nguvu ya ajabu sana.
Kutoka:23.25
Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Kutoka:23.26
Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.
Utumishi wa kumtumikia Mungu huleta baraka uzao wa matumbo na kuzuia uharibifu juu ya uzao wa matumbo.
Sasa sikia kama unatokea kwenye jamii ya watu ambao hawamchi Mungu , unatakiwa kuwa makini sana na ule mnyororo wa yale mazingira ,maana yale mazingira yanaweza kutumiwa kiroho na Shetani kupambana na wewe juu ya kupata uzao wa tumbo.
Hata kama umeokoka usije ukajiaminisha bure wakati unateseka na suala la uzao wa tumbo.
Hakikisha unatumia muda kuomba juu ya yale mazingira ya kwenye jamii yako , uenda yakawa yanatumiwa na Shetani kama kigezo cha kupambana na wewe juu ya kupata uzao.
Wewe simama kivyako na toba kwa ajili ya hayo mazingira ya kuto kumcha Mungu ,yaletayo utasa wa matumbo kwa watu walioko ndani ya hiyo jamii uliyotokea.
Aina ya maombi unayotakiwa kuyafanya ni maombi ya kujitenganisha na nguvu ya laana ya uzazi kutoka kwenye mazingira ya jamii ya watu wasio mcha Mungu kwa damu ya Yesu
Chukua muda wa kufanya toba ya kina halafu ukiweza shika tumbo lako na uanze kuliingizia damu ya Yesu huku ukilitamkia utakaso dhidi ya kila nguvu ya utasa iliyoshikilia hilo tumbo.
Kama ni mwanaume shika viuno vyako[Kuna somolitakuja juu ya kuombea viuno vya Mwanaume] na vimwagie damu ya Yesu na kuvitamkia utakaso kutoka kwenye hayo mazingira ya utasa ndani ya jamii yako.
Unaweza kuanza kuona tumbo likiwaka moto au ukitapika au likitetemeka sana au likiuma sana wala usiogope ,ujue hakika damu ya Yesu inapita ndani ya hayo mazingira yaliyotengeneza utasa ndani ya tumbo lako na kukutenganisha na hayo mazingira na baada ya hayo maombi usiache kutumia na sadaka kimaombi ukiweza ,kwa sababu saa zingine mazingira ya utasa toka ndani ya jamii yako isiyo mcha Mungu huwa yanatengeneza kwa sadaka wanazotoa kwa miungu au kwa roho za familia ,kwa hiyo na wewe simama na sadaka na useme maneno kinyume na utasa au laana ya uzazi toka ndani ya jamii yako.
Somo hili ni la muhimu sana kwa wapendao kutimizwa kwa makusudi ya Mungu duniani
Zaburi:139.13
Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi:139.14
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi:139.15
Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi:139.16
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Tunaendelea na aina za ufungwaji wa matumbo ya uzazi.
Neno la msingi ni hili 👇
Ayubu 3:10a;
"Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu."
Ikimaanisha kwamba milango ya matumbo ya uzazi inaweza ikafungwa kwa sababu mbalimbali.
Tuliona kuwa matumbo ya uzazi , kuwa yanaweza kufungwa kwa mazingira yaliyoko ndani ya jamii yako yale ya kuto kumcha Mungu
Na hilo tulilipata kwenye 👇
Ayubu:15.34
Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
Ayubu:15.35
Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu.
Inasema jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa
Jamii ya wasiomcha Mungu inaweza kubeba tabia ya kuharibika kwa mimba hovyo hovyo kulingana na hayo maandiko ya kwenye hiyo Ayubu.
Kuna ndugu aliolewa ndani ya jamii yenu kuabudu miungu sasa kwa sababu ya uchanga kiroho na kutokuelewa mambo yaliyoko ndani ya jamii ya mume ,alijikuta mimba zote zikiharibika na hakujua kwanini , na tulipokutana kwa maombi ,alishangaa sana kuona mapepo toka ndani ya jamii yake yakiripuka na kudai kuwa wameharibu maisha yake kupitia kupewa damu ya uzao wa tumbo lake na watu wa jamii ya mume wake.
Kumbe ndani ya ile jamii ya mume kuna mlango ambao umemtengenezea Shetani mazingira ya kuharibu mimba na kunywa damu ya uzao wa matumbo.
Mwingine nikaomba nae alikuwa ameokoka ndio lakini zile roho za upande wa jamii ya mume zilipochungulia kipaji cha mtoto baada ya kuzaliwa zikagundua mtoto wake hana chembechembe hata kidogo za mambo ya kwao ,zikaona utumishi wa Mungu ndani na sio utumishi wa roho hizo za familia ,zikamnyonga mtoto na akafa , hiyo ni aina ya milango toka ndani ya jamii yenye kumtengenezea Shetani mazingira ya kufuatilia uzao wa matumbo, kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa pia.
Mwingine anakuwa anateseka na swala la kupata uzao ,kumbe tatizo haliko kwa mume bali liko upande wa jamii ya mke ,mwingine tatizo linakuwa lipo upande wa jamii ya mwanaume na limepita kwenye viuno vyake na linapambana na swala la kupata uzao kwao.
Matatizo ya ufungwaji wa matumbo ya uzazi toka ndani ya jamii ,yanashughulikiwa kupitia damu ya Yesu.
Haijalishi jamii ya mume au mke imebeba roho gani na sheria zake za kupambana na upatikanaji wa uzao , bado damu ya Yesu inaweza kunena mema ,ni swala la imani tu na kuanza kuitumia juu ya kifungo cha kutoka ndani ya hiyo jamii.
Ukisoma 👇
Waebrania:2.14
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Waebrania:2.15
awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
Waebrania:2.16
Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
Utaona kuwa Yesu alishiriki mambo ya aina zote yahusuyo mwili na damu ili apate njia ya kutusaidia juu ya matatizo yahusuyo mambo ya mwili na damu, likiwamo tatizo la uzazi toka ndani ya jamii zetu leo.
Ndani ya mwili na damu ya Yesu kuna nguvu ya ajabu ya kutatua tatizo la kutokupata uazao.
Uwe umefungwa kwenye tumbo na kiunoni mwako toka ndani ya jamii ,mwili na damu ya Yesu ,vilishawahi kushiriki tayari hizo hali na imezishinda kabisa ooh haleluya ,baba ,mama yangu unahitaji uyahamini haya kabisa na yatakuwa ukombozi wako leo, Yesu alishawahi kuvaa mwili huu na damu kama mzao wa Ibrahimu na kama msomaji wa Biblia utagundua kuwa mzao wa Ibrahimu ulipitia changamoto ya kupata uzao kabisa ,Ibrahimu tumbo la mkewe Sara lilifungwa miaka mingi ,Rebeka mkewe Isaka alipata shida ya utasa pia ,mkewe Yakobo Raheli alikuwa tasa pia na Yesu alitokea ndani ya jamii ya namna hiyo pia lakini hii ni habari njema kwako Yesu alishinda hali zote za utasa ndani ya jamii yake na kwa sababu hiyo Biblia inasema kwenye 👇
Isaya:53.10
Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;
Utaona Biblia ikieleza kuwa kule kuchubuliwa kwa Yesu kiasi cha kumwaga nafsi yake yaani damu yake ,kulimfanya neno linasema Aone uzao wake na kuishi siku nyingi
Uzao wa Yesu duniani umepatikana kwa njia ya kuchubuliwa au kuumizwa mwili wake na kumwagika kwa damu yake msalabani.
Na kwa sababu hii pia Biblia inasema anaweza kuwasaidia pia na wote wanaopata shida ya kupata uzao.
Tazama Biblia inachokisema 👇
Waebrania:2.17
Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Waebrania:2.18
Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Inaeleza kuwa hakuna jambo tunalopitia ambalo Yesu hakupitia na kulishinda , hakuna mateso au mahangaiko ambayo unapitia leo ambayo Yesu hakuwai kupitia na kuyashinda ,kwa hiyo anajua namna ya kuyashinda ,ukimwendea na kumwamini ,shida yako ya kukosa uzao ataiondoa kabisa na utapata uzao kabisa.
Tukirudi tutakiangalia kifungo cha roho za wafu juu ya upatikanaji wa uzao na namna ya kukiombea.
Tutaendelea Kipindi Kingine.....
0 Comments