UZINIFU KWA WATUMISHI

NI KWANINI BAAZI YA WATUMISHI WA MUNGU NI WAZINIFU❓

     Gabo Zigamba na Christina Shusho

Nimeulizwa swali hili na mpendwa mmoja na majibu yangu ni kama ifuatavyo.


1.Hao watumishi si wateule wa Mungu


Biblia inasema hivi


👉Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.


⛔Wateule wa Mungu hawawezi kufanya dhambi ya uzinzi✔


2.Hao watumishi hawaongozwi na nguvu za Roho mtakatifu


Imeandikwa hivi


👉Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.


⛔Wanaoongozwa na Roho mtakatifu hawawezi kufanya dhambi ya uzinzi✔



3.Hao watumishi hawana kweli ya Mungu ndani yao.


Imeandikwa hivi


👉Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.


⛔Kama mtu hana kweli ndani yake ni rahisi kuanguka katika dhambi ya uzinzi✔


4.Hao watumishi hawamjui Mungu wanayemtumikia


Imeandikwa hivi


👉Tito 1:16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.


⛔Mtu anayemjua Mungu anayemtumikia hawezi kutenda dhambi ya Uzinzi✔


5.Hao watumishi fikra zao zimepofushwa na yule mwovu shetani


Imeandikwa hivi


👉2 kor 4:4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


⛔Mtu aliyepofushwa fikra zake hawezi kumpendeza Mungu, na wala hawezi kuishinda dhambi ya uzinzi✔


6.Hao watumishi bado hawajazaliwa Mara ya pili


Imeandikwa hivi


👉1 Yohana 3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.


⛔Aliyezaliwa mara ya pili  hawezi kufanya dhambi ya uzinzi.✔


7.Hao watumishi hawajaishinda nia ya mwili


Biblia inasema hivi


👉Warumi 8:7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.


⛔Kama mtu hajaishinda nia ya mwili hawezi kuishinda dhambi ya uzinzi.✔


8.Hao watumishi hawana mazoea ya kufunga na kuomba mala kwa mala


Imeandikwa hivi


👉Mathayo 26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.


⛔Mtu asiye na mazoea ya kufunga na kuomba mala kwa mala ni rahisi kuingia majaribuni na ni rahisi kuanguka katika dhambi ya uzinzi.✔

➡Hizi ni miongoni mwa sababu zinazopelekea Mtumishi au mtu kuanguka katika dhambi ya uzinzi.


🔶USHINDI.


KUFANYA TOBA YA KWELI NA KURUDI KATIKA NJIA SAHIHI ZINAZOKUWEKA MBALI NA DHAMBI YA UZINZI

Mwisho.

👉Ufunuo 2:5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Mungu awabariki sana🙏

Post a Comment

0 Comments