ROHO YA UTASA SEHEMU YA 1 (MTUMISHI ANORD)



UTANGULIZI.

KUTOKA KWA MTIMISHI ANORD

Wapo watu wanaopitia magumu sana yakutokupata watoto, Wengine hadi wamefikia kuachana hasa katika ndoa. Utasa husababishwa  na mambo mengi sana. Yapo pia yenye uhalali na yasiyo na uhalali.Tutajifunza kwa mapana zaidi na hiyo roho ya utasa lazima ipigwe ili Kristo Yesu akupe chema. Lakini cha ajabu Mungu anapowatendea watu muujiza huu wakishamaliza hata kumshukuru Mungu hakuna , utawaona siku ya kutafuta mtoto wa pili! Ni vyema kumshukuru Mungu.Roho ya utaswa haitatuliwi kwakwenda kwa mganga , Ni Yesu pekee! Wapo walioenda kwa waganga wakapata watoto, unadhani watoto hawa watakuwa na sifa gani? Basi tujifunze utapata majibu yote. 

Kusudi la Mungu kwa mwanadamu ni kuzaa na kuongezeka. Kwahiyo roho ya utasa ni mpango wa Shetani na siyo wa Mungu wetu.

Utasa ni roho kamili kabisa kwenye maisha ya watu. Ni roho ambayo wachawi wanaweza wakakutupia ili ubaki kwenye uharibifu.

Utasa ni kifungo kamili ambacho Shetani na mawakala wake hukitumia ili mtu asisonge mbele kwenye baraka zake.

Kuna aina mbili za Utasa.
1.Utasa wa kimwili
2.Utasa wa kiroho

“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
  Mwanzo.  1:28   

“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
  Efeso 1:3   

“Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.”
  Kut.   23:26   

“Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA.”
  Mwa.   25:21-22   

“Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.”
  Isa.   66:9   

“Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo. Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.”
  Kumb.   7:14-15   

“Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo; yaani, hiyo huja katika ubatili, na huenda gizani, nalo jina lake limefunikwa giza;”
  Mhu.   6:3-4   

“Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe. Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani.”
  Ayu.   3:7-8   

“Kwa kuwa utasahau mashaka yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita; Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri.”
  Ayu.   11:16-17   

“Vitisho vimenigeukia; Huifukuza heshima yangu kama upepo; Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.”
  Ayu.   30:15   

“Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;”
  Isa.   46:3   

“Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.”
  Omb.   3:31-33   

“Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.”
  Mith.   8:17   

“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”
  2 Kor.   8:9   

“Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.”
  Gal.   4:27   

“Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; Lakini kwa

harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.”
  Ayu.   14:7-9  

“Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea.”
  2 Fal.   2:19-20   

“Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.”
  1 Fal.   3:17-22  

“angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.”
  Yer.   1:10   

“Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.”
  Mt.   15:13   

“Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”
  Uf.   5:9-10  
Jube ni jini linalosimamia roho ya utasa kwenye maisha ya watu Sumiri anasemamia kuangamiza mimba,Uvimbe wa tumbo.

“Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”
  1 The.   2:18   .

Kama hupati mtoto, au hujapata mtoto hakikisha tunawasiliana tuweze kutengeneza kwa jinsi ya Rohoni na kumsihi Mungu akupe mtoto.Hii ni kwa Wanandoa usije hujaolewa halafu unataka mtoto, Elewa hili!Na sio ndoa za rejareja au mkeka, ndoa takatifu. Kumbuka hili andiko ;

Kutoka 23:26   

“Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.”


Tutaendelea sehemu ya pili.....

Post a Comment

0 Comments