Pongezi nyingi kwako msichana uliyepewa mimba na kutelekezwa lakini hukuitoa bali uliamua kuilea na kuendelea kumlea mtoto wako peke yako bila hata ya msaada wa baba wa mtoto. Wamama wengi ambao hulea mtoto au watoto bila kuolewa maranyingi huonekana kama hawapo sawa kulingana na mfumo wa jamii. Jamii imekuwa ikiwa judge bila kujua nini wamepitia na wanapitia. Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanapaswa kulelewa na wazazi wawili lakini hii siyo sababu ya kumdharau msichana anayalea mtoto mwenyewe maana hujui nini kimepelekea hali hiyo.
Mungu awabariki sana na awakumbuke pamoja na watoto wenu. Usikate tamaa wala kujenga chuki na kisasi na baba wa mtoto, wewe endelea kuangalia maisha ya mtoto wako na kuboresha maisha yako na hakika Mungu hatakuacha na atakupa haja za moyo wako. Sisi wenye ndugu na marafiki ambao ni single mothers tujue wanatuhitaji kuwakubali, kuwatia moyo na kutowajudge. Kama hajaamua kukuambia baba wa mtoto heshimu maamuzi yake na sio kila saa kumsumbua kwa maswali.
*MUNGU AWABARIKI SANA*
0 Comments