KWA VIJANA WA KIUME NA WANAUME HII YA MUHIMU SANA

KWA VIJANA WA KIUME NA WANAUME, HII YA MUHIMU SANA
(NI NENO LA MUNGU KWAKO).

Wanaume Na Watoto Wa Kiume Wanadhani WANAOPATA HASARA Kutokana Na UASHERATI NA UZINZI Ni Watoto Wa Kike Eti Kwa Vile 'INABAKI ALAMA KUONESHA KUWA AMETUMIKA' ... Basi Kwa Kuwa Huwezi Jua Kuwa Mwanaume Amejitunza Au Ni Mzinzi Kwa Vile HAIBAKI ALAMA Baada Ya Kutenda Dhambi Ya UZINZI AU UASHERATI, Wanaume Wengi Wamekuwa Wakiona SWALA LA KUJITUNZA NA KUJIHESHIMU Ni La Watoto Wa Kike Tu, Hii Si Kweli Ni Uongo Wa Shetani Kujaribu KUHARIBU HATMA ZETU Kwa KUTIA GIZA Kwenye AKILI ZETU Ili TUJIMALIZE WENYEWE Kupitia Dhambi Hii!

Leo Nataka UONE NINI UNAPOTEZA Unapozini Au Kufanya Uasherati, Kwa Mujibu Wa Neno La Mungu;

"USIWAPE WANAWAKE NGUVU ZAKO; Wala Moyo Wako Usiwape Wale Wawaharibuo WAFALME" (Mithali 31:3).

Hii Ina Maana Kuwa KILA UNAPOZINI NA MWANAMKE, UNAPOTEZA NGUVU... Hii Nguvu Mungu Anayoisema Si NGUVU ULIYOPOTEZA WAKATI WA KUFANYA HICHO KITENDO PEKE YAKE [JAPO NAYO INAPOTE]... Ziko NGUVU ZA AINA NYINGI AMBAZO UNAPOTEZA, TUONE BAADHI YA HIZO HAPO CHINI;

1.NGUVU YA KIAKILI;

"AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA..." (Mithali 6:32).
Kila UNAPOZINI Kuna Kiwango KIKUBWA SANA CHA AKILI KINAONDOKA NDANI YAKO... Hii Ndiyo Sababu Iliyomfanya YUSUFU Akatae KUZINI NA MKE WA POTIFA; Alijua Ana MAONO MAKUBWA MBELE YAKE, YANAYOHITAJI AKILI NYINGI NA KUBWA, NA MSAADA WA AKILI ZA KIMUNGU, Ndipo Akamjibu Mke Wa Potifa, "NIFANYEJE UOVU HUU MKUBWA NIMKOSE MUNGU?"
Biblia Haisemi ANAYEZINI HANA AKILI, Hapana... Inasema "HANA AKILI KABISA" Yaani NI TAAHIRA, NI MWEHU...Maana Angejua HASARA ATAKAYOIPATA KISA STAREHE YA DAKIKA KADHAA, ASINGEFANYA HUO UPUUZI!

2.NGUVU YA KUPATA UTAJIRI;
"NAWE UTAMKUMBUKA BWANA MUNGU WAKO AKUPAYE NGUVU ZA KUUPATA UTAJIRI" (Kumbukukumbu La Torati 8:18).
Kati Ya Vitu Ambavyo UZINZI NA UASHERATI Huaribu Ni Eneo La NGUVU YA KUPATA UTAJIRI AMBAYO MUNGU AMEWEKEZA NDANI YAKO... Kila UNAPOZINI NA KUFANYA UASHERATI, KUNA NGUVU YA KUUPATA UTAJIRI UNAIUZA...UNAUZA UTAJIRI NA KUFUNGUA MLANGO WA ROHO ZA UMASIKINI NA KUTOFANIKIWA NA KUKOSA HESHIMA VIINGIE MAISHANI MWAKO!

3.NGUVU YA UTAKATIFU NA UJASIRI WA KUMSOGELEA MUNGU;

"WAOVU HUKIMBIA WASIPOFUATIWA NA MTU [WASIPOKIMBIZWA NA MTU]; BALI WENYE HAKI NI WAJASIRI KAMA SIMBA" (Mithali 28:1).
Waovu, Watenda Dhambi Ikiwemo Uzinzi, Ni WAOGA NA WENYE HOFU, Hawana UJASIRI NA NGUVU NDANI YAO YA KUMSOGELEA MUNGU, Kwa Maana KILA MARA ADUI, SHETANI ANAWAHUKUMU NA KUWASHTAKI MOYONI MWAO Kuhusu DHAMBI YAO... Dhambi Zingine Zote Ni RAHISI KUZIONDOA KWENYE AKILI YAKO, Lakini DHAMBI YA UZINZI ILIYOFANYIKA MWILINI MWAKO, Haiondoki Kirahisi Kwenye AKILI YAKO, Na Shetani Ataitumia Kila Muda Kukuonesha JINSI ULIVYO MCHAFU, Na Jinsi Ambavyo HAUFAI MBELE ZA MUNGU... Na Hapo Ndipo NGUVU YA KUMSOGELEA MUNGU NA UJASIRI HUONDOKA...Shetani Hukuonesha JINSI ULIVYO MCHAFU NA MTUPU, Maana Tayari UTUKUFU WA MUNGU UMEONDOKA JUU YAKO... Na Nguvu Ya Utakatifu Na Ujasiri Vikiondoka Ndani Yako, INAKUWA SI RAHISI KUMSOGELEA MUNGU!
Na Mlango mkubwa Shetani Anaotumia Kukushambulia Na Kukudhoofisha Ni MLANGO WA ZINAA!

4.NGUVU YA KUZIKABILI TAABU/ MAGUMU YA MAISHA;

Neno La Mungu Linasema, "AZIMIAYE SIKU YA TAABU, NGUVU ZAKE NI CHACHE"

Kumbuka Andiko Letu La Msingi Kwenye Mithali 31:3, Kila UNAPOZINI UNAPOTEZA NGUVU... Na Hiyo Nguvu Uliyopoteza Inakuwa Imewekwa MAALUM Ndani Yako Na Mungu Kwa Ajili Ya KUZIKABILI CHANGAMOTO/ MAGUMU NA TAABU ZA MAISHA.
Nguvu Zako Zikiwa Chache, Lazima Utazimia Siku Ya Taabu!
Kila Unapozini Nguvu Inapotea, Kila Unapotenda Dhambi, Nguvu Inaondoka, Na Mwisho Wa Siku Changamoto Za Maisha Zinaanza KUKUGARAGAZA Na Hata Kufikia Hatua Ya KUKOSA THAMANI YA MAISHA!

Naamini Mungu Amekupa Kitu Mwanaume Na Mkaka Mwenzangu

Post a Comment

0 Comments